Thursday, March 13, 2014

KANUNI ZA UANDISHI WA KAMUSI

               







          











                                     KANUNI ZA UANDISHI WA KAMUSI                                                                                                                                                                                                  
                                                       NA Kapele. H                                     
                                                                                                                       

Karibuni tena wadau, wapenzi na watetezi wa lugha adhimu ya Kiswahili ambayo kwa sasa Chama Cha Wanafunzi wanaosoma Kiswahili Afrika Mashariki na Kati (CHAWAKAMA) wamejizatiti kuitunza na kuiendeleza, kwa upendo wa dhati kabisa wamepiga hatua moja mbele  ya kufanya maamuzi ya kubeba maandishi migongoni mwao yenye kauli mbiu kuwa KISWAHILI NI TUNU NA JOHARI YA AFRIKA. Leo hii naileta kwako lugha hii ikiwa na mengi yahusuyo kanuni za uandishi wa kamusi. Kazi ni kwako kuitalii na kuweza kutoa hukumu kama kweli Kiswahili ni Tunu na Johari ya Afrika?

Katika kuijadili mada hii ni vema tuanze kwanza na fasili muhimu ambazo ndio msingi na muhimili mkuu na njia ya kutufikisha kule tunakotaka kufika. Kama wanavyosema watu wengi kuwa bahari haivukwi kwa kuogelea na tena mti ukuliao kivulini sio thabiti basi na tuanze.
UTUNGAJI: Ni dhana pana na telezi hususani isipowekwa katika muktadha maalumu; matumizi ya dhana hii yasipowekwa katika muktadha maalumu yanaweza kuchanuza maana nyingi na tofautitofauti kama vile:
i.       kitendo cha kupitisha uzi, ung’ongo kwenye kitu chenye tundu.
ii.     Kusanyika kwa kitu kiwowevu kama vile usaha au maji katika mwili.
iii. Unganika kwa mbegu ya uzazi ya kiumbe wa kiume katika sehemu ya uzazi ya kiumbe wa kike.
iv.    Toa mawazo kutoka bongoni na kuyakusanya, kisha kuyadhihirisha kwa maandishi pia tunga yaweza kuwa dunga.

Katika muktadha huu wa kanuni za uandishi wa kanuni za kamusi. Utungaji utakaoshughulikiwa ni ule unaohusu utayarishaji au uandishi wa kamusi.
(TUKI, 2012:617), wanaeleza kuwa utungaji ni namna au jinsi ya kutunga. Kutunga ni neno lililotokana na neno tunga hivyo linaweza kufasiliwa kuwa ni kitendo cha kutoa mawazo bongoni na kuyakusanya kisha kuyadhihirisha kwa maandishi kimasimulizi, kimziki nk.




 KAMUSI: ni mkusanyiko wa maneno ya lugha moja au zaidi ambayo mara nyingi huorodheshwa kialfabeti yakiwa na maelezo ya matumizi yake, fasili na historia ya maneno, matamushi na maelezo mengine. MDEE (2007:81) kamusi ni hazina ya lugha inayohusika, kwani ni tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa na orodha ya maneno mbalimbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile pamoja na maana zake. kutokana na umuhimu wa kamusi watu wengi wanaojua kusoma na kuandika huwa na kamusi ofisini au shuleni kwa ajili ya kuitumia pale wanapoihitaji. 

Zgusta (1971), anafasili kuwa  kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa mzungumzaji wa jamii fulani kupangwa kwa utaratibu maalumu kisha kufafanuliwa kwa utaratibu ambao msomaji anaweza kuelewa.

Bwenge (1995), msamiati unaoingizwa katika kamusi unatokana na jamii fulani. Ufafanuzi unaongezwa katika kamusi ni ule unaohusu fasili na maelezo mengine kulingana na malengo ya kamusi inayohusika. Maelezo hayo yanatiwa mashiko zaidi na mtaalamu Kipfer (1984), kuwa ni maumbo, matamshi, matumizi, maana, historia ya maelezo na matumizi ya kinahau ya kidahizo.

TUKI (2004), wanafasili kuwa kamusi ni kitabu cha maneno yaliyopangwa kwa utaratibu wa alfabeti na kutolewa maana na maelezo mengine.

Nielsen (2008), kamusi inaweza kutazamwa kama zao la lekskolojia ambalo lina sifa kuu tatu ambazo ni;
i.                Kuandaliwa kwa ajili ya kazi moja au zaidi.
ii.             Huwa na data zilizochanganiliwa kwa lengo kutimiza kazi hizo.
iii.          Huwa na muundo ambao ni kiungo na unaweka uhusiano baina ya data ili ziweze kutimiza mahitaji ya mtumiaji.

Mdee na wenzake (2011), kamusi ni kitabu cha maneno yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana na maelezo ya matamshi, taarifa za kisarufi n.k kwa kila neno. Fasili hii si tofauti na fasili aliyoitoa Mdee (2007:81), kamusi ni kitabu cha maneno pamoja na maelezo ya maana za hayo maneno. Kamusi huweza kuwa ya lugha moja, yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo ya maana yake yakiwa katika lugha moja kama ilivyo katika kamusi ya Kiswahili sanifu.

MAMBO YANAYODOKEZWA NA WATALAAMU
Katika fasili mbalimbali za wataalamu hawa yapo baadhi ya mambo muhimu ambayo yamekudokezwa. Mambo hayo ni pamoja na:
  •        Kamusi huwa na maneno ambayo yamepangwa kwa utaratibu maalumu.
  •      Lazima kuwe na maneno yaliyo katika orodha.
  •      Maneno hayo lazima yatolewe maelezo fulani.


UDHAIFU WA FASILI
i.                    Utaratibu maalumu haujaelezwa.
ii.                 Upangaji wa maneno katika kamusi kwa kikoa cha maana kimesahaulika.
iii.               Mifumo ya kielekroniki hakijazungumzwa.
Kwa ujumla kamusi inaweza kufasiliwa kuwa ni orodha ya maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu au yaliyo katika mfumo wa kielektroniki yaliyopangwa kialfabeti au kivikoa pamoja na maelezo yanayofafanua maana ya maneno hayo, asili na historia, matamshi, kategoria, mifano ya matumizi, mitindo ya matumizi n.k

UTUNGAJI WA KAMUSI
Taaluma inayohusu utungaji wa kamusi huitwa lekskografia na neno lekskografia limetokana na maneno mawili ambayo ni
i.                    lexcal-lenye maana ya taluma ya kisayansi.
ii.                 Grafia-lenye maana ya sanaa.

Hivyo basi lekskografia ni kazi ya kisayansi na kisanaa ya kutunga kamusi inayojumuisha uorodheshaji wa msamiati wa lugha inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo ya kufafanua neno lililoorodheshwa kadri ya watumiaji wa kamusi iliyotungwa. Lekskografia kama taaluma ya utungaji wa kamusi ni kazi ya kisayansi na kisanaa ya utayarishaji au uandishi wa kamusi kwa ujumla.

Uandishi wa kamusi ni mchakato kwa sababu unahusisha hatua zifuatazo:  

  • Kupanga na kusanifu mradi. Katika hatua hii ni vema kuhusisha jopo kwa sababu sehemu hii inahusisha mambo mengi sana hivyo sio rahisi kwa mtu mmoja kuifanya kazi hii. Kwani mradi unaweza kufikiwa wakati thamani yake imepungua kwa maana ya kuchelewesha mahitaji ya watumiaji ambayo yanawezakusababisha kupotea kwa wahitaji.



  •     Kufanya utafiti, katika hatua hii ni muhimu sana kujiuliza swali kabla ya kuanza kuiandaa kamusi. Mwanalekskografia anapaswa kufanya utafiti wa kina juu ya kamusi gani inahitajika katika kipindi ambacho jamii inapitia. Katika utafiti kuna hatua muhimu zinapaswa kufuatwa.


  •     Ukusanyaji wa msamiati, mara tu baada ya kufanya utafiti na kupata matokeo ya utafiti mwanalekskografia nahitajika kukusanya msamiati yaani jumla ya maneno yanayotumika.


  • Kuandika na kuhariri, hatua hii mwanalekskografia anatakiwa kuandika na kuhariri kamusi ili kuwa na mradi uliokamilika na wenye kuwa na mvuto kwa mtumiaji.


  •       Kuchapisha ni hatua ya mwisho kabisa katika mchakato huu wa uandishi wa kamusi.


Kwa hatua hizi napenda kuwapongeza TUKI kwa sasa TATAKI kwa kufuata hatua hizi za uandishi wa kamusi ya Kiswahili sanifu ambayo ina jumla ya matoleo matatu mpaka sasa. Matoleo haya yanamchango mkubwa kwa mtumia lugha kuongeza msamiati. Mgawanyo wa vipindi vya kamusi sanifu ni pamoja na kipindi cha baina ya 1964-1981, kipindi cha baina ya 1981- 2004, kipindi cha baina ya 2004-2012.






MSAMIATI: ni maneno yanayotumika katika lugha fulani. Kwa muktadha huu neno hili haliana wingi bali umoja tu. Au ni orodha ya maneno yaliyochaguiliwa kutoka lugha ya kawaida au lugha ya fani fulani na kupewa maelezo mafupi ya maana za maneno hayo. Hivyo maneno yote yaliyo katika fani fulani ndiyo msamiati wa fani hiyo.
Neno msamiati huweza kuwa na wingi endapo tunazungumzia maneno kutoka fani mbalimbali. Mfano: siasa, kilimo, uvuvi, n.k ingawa lugha  huwa na maneno mengi, mtungaji huteua msamiati kutegemea na malengo yake kwa kuacha mwingine.

VIGEZO VYA UTEUZI WA MANENO
i.                    Kigezo cha umbo la neno.
ii.                 Kigezo cha maana ya neno.
iii.               Kigezo cha historia ya neno.
iv.               Kigezo cha matumizi ya neno.
                                                                            Imehaririwa na kapele.H  



   

    

No comments: