TANGAZO!!!
CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU
AFRIKA MASHARIKI
(CHAWAKAMA)
KINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WADAU
WOTE WA KISWAHILI KUWA:
KONGAMANO LA KUMI (10) LA
KIMATAIFA LA KISWAHILI NA MKUTANO MKUU LINATARAJIWA KUFANYIKA NCHINI KENYA
TAREHE 21/08/2014 – 24/08/2014.
KUHUSU NCHI
- KENYA
KUHUSU CHUO
- LAIPIKIA
KUHUSU TAREHE - 25/08/2014 HADI 27/08/2014
KUHUSU SIKU YA KUWASILI- 24/08/2014
KUHUSU GHARAMA ZA KONGAMANO
·
MALAZI KWA SIKU NNE - TSH 12,000
·
CHAKULA -TSH 24,000
·
FULANA -TSH 15,000
·
CHETI CHA USHIRIKI -TSH 4,000
JUMLA YA GHARAMA = TSH 55,000
GHARAMA ZOTE HAPO JUU ZIKABIDHIWE KWA
KIONGOZI WA TAWI KABLA YA 20/07/2014.
KUHUSU
NAULI: KILA MSHIRIKI ATAJITEGEMEA KWANI MAZINGIRA
YA MWANZO WA SAFARI YATATEGEMEA NA MSHIRIKI ANAKOSOMA AMA ANAKOISHI. ILA
MCHANGANUO WA NAULI NI KAMA IFUATAVYO:
WASHIRIKI WATAKAOANZIA SAFARI DAR ES SALAAM, MOROGORO WANATAKIWA KUANDA
TSH 134,000 KWENDA NA KURUDI, AMBAPO WASHIRIKI TOKA MBEYA WATATAKIWA KUUNGANA NA WASHIRIKI TOKA DAR ES SALAAM, MOROGORO, IRINGA, DODOMA, NA MIKOA JIRANI. KWA
WASHIRIKI WA MWANZA TSH.114000 WAO WATATAKIWA KUPITIA MPAKA WA UGANDA HIVYO SI MUHIMU KWAO
KUPITIA DAR ES SALAAM. Arusha tsh.54000 kwenda na kurudi.
KUHUSU
HATI YA KUSAFIRIA (PASIPOTI)
KILA MWANACHAMA ANATAKIWA KUWA NA HATI YA
KUSAFIRIA KATI YA HIZI:
Ø HATI NDOGO (PASIPOTI NDOGO) TSH. 10,000
Ø HATI KUBWA YA KUSAFIRIA (PASIPOTI KUBWA)
TSH.50,000
KILA MMOJA
ATALAZIMIKA KUFIKA OFISI ZA UHAMIAJI ZILIZO KARIBU NA MAKAZI YAKE ILI
KUKAMLISHA MCHAKATO WA HUO.
KAULI MBIU
YA KONGAMANO NI
“KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI”
Kauli mbiu hii inalenga kuhimiza umoja na utangamano wa nchi za
Afrika Mashariki.Lugha ya Kiswahili ina mchango mkubwa sana katika kuleta
utangamano,umoja na mshikamano mwema baina ya nchi za Afrika Mashariki.Kando na
mchango wa Biashara,Michezo na
Elimu.Swali ni je,Lugha ya Kiswahili ina mchango wowote katika mchakato wa
kuimarisha na kukuza vipengele hivi vitatu; umoja,utangamano na mshikamano.
MADA ZA KONGAMANO
1. Kiswahili ni lugha mwafaka
ya umoja wa Afrika mashariki.
2. Nafasi ya lugha ya
Kiswahili katika tamaduni za nchi za Afrika Mashariki.
3. Kiingereza au Kiswahili?
Katika mwamko mpya wa Afrika Mashariki huru.
4. Kiswahili na michakato ya
kisiasa katika nchi za Afrika mashariki.
5. Nafasi ya Kiswahili katika
sanaa ya kisasa (Karne ya ishirini na moja).
6. Mchango wa lugha ya
Kiswahili katika upanuaji na uendelezaji wa elimu
ya juu Afrika Mashariki.
7. Kiswahili na uimarishaji
wa usalama katika ubia Afrika mashariki.
8. Changamoto za
kisiasa,kiuchumi na kiusalama katika lugha ya Kiswahili,
9. Ubunifu na talanta katika
uzalishaji wa kazi mufti ya fasihi ya Kiswahili
Lugha ya Kongamano:
Lugha rasmi ya Kongamano ni Kiswahili. Makala yaliyoandikwa kwa
Kiingereza yatakubaliwa tu iwapo hapana budi.wajumbe wanashauriwa kuanda makala
yao katika lugha ya kiswahili
Ikisiri: Ikisiri za kati ya maneno 200-300 zitumwe kabla ya tarehe
30 Mei 2014 kwa Mratibu wa Kamati ya Maandalizi kupitia barua meme kwenye anwani
ifuatayo:Billysakwa@gmail.com,AU Mhariri
Mkuu godwinalex664@yahoo.com (+255718252853) au kwa katibu mkuu wa
chawakama Afrika mashariki Ahamadi Jumbe. Chawakama.am@gmail.com.
Makala: Makala kamili ya ikisiri zitakazokubaliwa yatumwe kwa
Mratibu kwa baruameme kufikia tarehe 30 Juni 2014 kupitia anwani ifuatayo:
Billysakwa@gmail.com
Ili kupata nafasi ya kuwasilisha makala uliyoandaa ni lazima.mjumbe
atume ikisiri na hatimaye makala kamili ya mada aliyoandaa.Makala haya
yatachapishwa katika chapisho la makala la kongamano kabla ya tarehe 15 Julai
2014 .utaratibu na mpangilio wa uwasilishaji utatolewa tarehe 30 Julai 2014.
“KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI”
No comments:
Post a Comment