KHAMZIA
Kuna tanzu mbili za ushiri wa
Kiswahili na ambazo zimetokana na asili ya kiarabu. Tanzu hizi ni “takhamisa”na
“khamzia”.
Utungo wa takhamisa una mistari mitano. Ilivyo ni kwamba utungo huu hutungwa na
watu wawili. Mshairi wa kwanza hutunga mistari miwili ya mwisho na yule wa pili
hutunga mistari mitatu ya kwanza lakini kwa kutumia kina cha mstari wa kwanza
kati ya ile mistari miwili iliyotungwa na yule mtu wa kwanza.
Lakini katika utungaji yahitajia
kwamba ile mistari ya mwanzo itakayongezwa isiharibu maana iliyoukiliwa na
kwamba iwapo ile mistari mitatu itaondolewa ile miwili ibaki na maana yake ile
ya mwanzo.
Utungo wa hamziya
wahitaji mambo matatu muhimu, kwanza kabisa utungo huu unakuwa ni mistari
miwili miwili, pili utungo jinsi ulivyo mistari yake haigawanyiki
katika
vipande viwili. Tatu ni kwamba silabi ya mwisho ya mstari wa kwanza si
lazima iwe sawa na silabi ya mwisho ya mstari wa pili, lakini silabi
zake za mwisho katika mistari yote ya mwisho shurti zilandane au ziwe na urari.
(makala
za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili III, fasihi 2003:64-65)
Mashari aina ya takhimisa na hamziya yana asili ya kiarabu na tathlitha au utatu umetokana na
nyimbo za Kiswahili. Hamziya ni fasihi andishi ya kwanza ambayo ilitafsiriwa
kutoka kiarabu mnamo mwaka 1652,
kuhusu maisha ya mtume Muhamadi. Hamziya ilivumbuliwa huko pate. Ingawa hamziya
ilitafsiriwa kutoka kiarabu lakini ina muundo wa kibantu na lugha iliyotumiwa
ina misingi mikubwa ya familia ya kibantu. Ni wimbo kwa ajili ya mtume wa kiislam
na uliimbwa kwanza kabisa huko Egypt
katika karne ya 13.
No comments:
Post a Comment