Friday, December 20, 2013

KONGAMANO LA KANDA YA TANZANIA-2014, TANGA

UONGOZI WA CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA
BARUA PEPE; chawakama2004@yahoo.c0m,  eeliase43@yahoo.com
Namba za simu; 225752808157, 225714676035, 225769804017, 225757487481.

UNAPENDA KUWATANGAZIA KUWA KONGAMANO LA SITA (6) LA CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA LITAFANYIKA KATIKA CHUO KIKUU CHA ECAMFORD MKOANI TANGA TAREHE 26 FEBRUARI, 2014 HADI 29 FEBRUARI, 2014

KONGAMANO LITAHUSISHA YAFUATAYO:

KUWASILISHA MADA NNE, MADA YA MWISHO ITAWASILISHWA UFUKWENI ALIKOKUWA AKIUZIA VITABU HAYATI SHABAN ROBERT KAMA TUKIO LA KUMUENZI.
KUNTU YA HILO PIA TUTAZULU NYUMBANI KWAKE, ALIKOZIKWA NA MAKTABA YA VITABU VYAKE ILIYOFUNGULIWA HIVI KARIBUNI
KUTEMBELEA MAENEO YA MAKUMBUSHO PANGANI NA MAPANGO YA AMBONI
SEUZE YA HAYO, KUTAKUWA NA WAIGIZAJI NA VIKUNDI VYA SANAA
MRISHO MPOTO
MZEE MAJUTO
BENDI MOJA YA MUZIKI WA TAARABU
PIA ATAKUWEPO MBUNGE WA MONDULI MHE. EDWARD LOWASSA, VIONGOZI WA KISERIKALI, MANGULI WA LUGHA KISWAHILI NA VYOMBO VYA HABARI
TUNATEGEMEA PIA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA USAFI MJINI TANGA KAMA ILIVYO UTAMADUNI WAO
GHARAMA ZA JUMLA ZA KONGAMANO NI SH. 56000/=
CHAKULA KWA SIKU NNE SH. 20500/=
MALAZI                                        SH. 10000/=
CHETI                                             SH. 6000/=
FULANA                                        SH. 12000/=
SAFARI ZA NDANI                     SH. 7500/=
TANBIHI;
KILA MWANACHAMA ATAJITEGEMEA NAULI YA KWENDA NA KURUDI
GHARAMA ZA KONGAMANO ZITOLEWE MAPEMA ILI KULETA UFANISI, MWISHO WA KUPOKEA FEDHA NI TAR. 10/01/2014. BAADA YA HAPO UONGOZI HAUTOPOKEA MCHANGO WOWOTE.
WANACHAMA MNAOMBWA KUTUMA MADA KABLA YA TAREHE 05/01/2014
KAULI MBIU; “MIAKA 52 YA UHURU, KISWAHILI TUNU YA KIJANA KWA MAENDELEO ENDELEVU”

IMETOLEWA NA,
LUGWISHA ELIAS LUDOLI
KATIBU MKUU, CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA.

KUPITIA MWENYEKITI WA TAWI CHAWAKAMA-TEKU
KAPELE HARRY-0763891415.

SHIME WANATEKU TWENDENI TANGA KUJIFUNZA NA KUKITANGAZA CHUO NA TAALUMA ZETU.





No comments: