ISTILAHI ZA USHAIRI - tarehe 9/5/2013
MAANA YA ISTILAHI
Ni maneno
yanayotumiwa katika tathinia fulani, hivyo katika taaluma ya ushairi kuna
istilahi muhimu zitumikazo katika kuunda na kujenga ushairi wa Kiswahili.
Istilahi hizo ni:
- Arudhi
Ni
sheria na kanuni za kimapokeo, jadi au kitamaduni zinazoongoza utunzi
wa mashairi, tenzi, na ngonjera. Kanuni
hizo zaweza kuwa ni vina, mizani,
beti, mishororoau mistari, kituo, kibwagizo,
mikarara, utoshelevu, muwala
na lugha safi.
- Bahari
Ni kina kinachotokeza mwishoni mwa
mshororo wa beti.
- Ubeti
Ni mgawo wa vifungu katika shairi,
utenzi, au ngonjera unaojitosheleza
kimaana. TUKI
(2003:94), wanaeleza kuwa: ubeti ni kifungu chenye kuleta maana kamili katika jumla ya vifungu
vilivyomo katika utungo.
Mfano:
Kaa kaa kwenye kiti, kaa na kaa wa
pwani,
Kaa ni la moto binti, nisikiza kwa
makini,
Kaa waambiwa keti, ewe bwana una
nini?
Huu ni ubeti mmoja katika utungo wa shairi
letu kutoka katika Mzenga, (2010:4)
- mshororo
ni mstari katika ubeti wa shairi ambao
una maana kamili. Katika mashairi
ya arudhi inatakiwa mistari iwe sawa
kimizani ingawa baadhi ya mashairi
huwa yanakuwa na mizani tofauti.
Mfano:
Paa ni la kuezeka, kwenye nyumba pulikani.
Huu
ni mshororo mmoja wenye mizani kumi na sita.
- mwanzo
ni mshororo wa kwanza katika ubeti wa
shairi. Katika tarbia mshororo wa
kwanza huitwa
ufunguo au fatahi au kifunguo.
Buibui
ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Nyumba iso mlingoti, na wala
vipachikiyo,
Toka pembe hadi kati, yote ya
mning’iniyo,
Haiezekwi makuti, na wala
kifunikiyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Ubeti
wenye wino mzito ni mfano wa mwanzo wetu katika utungo wetu.
- mloto
ni mshororo wa pili katika ubeti wa
ushairi.
Mfano:
Buibui ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Mstari wenye
wino mzito kishairi huo ni mroto.
- mleo
ni mshororo wa tatu katika ubeti wa
shairi.
Mfano:
mja deni utalipa, hata likiwa ni mia,
dawa ya deni kulipa, wala siko
kukimbia,
deni harusi kukopa, kulipa wafikiria,
ili moyo uwe shwari, mja kamilisha
deni.
Mleo umekolezwa zaidi ya mishororo mingine
katika ubeti.
- kituo
ni mshororo wa mwisho katika ubeti
wa utungo wa ushairi. Maneno ya kituo
yanaweza yakawa yale yanayokaririwa katoka
ubeti hadi ubeti yaani kibwagizo.
Pia yanaweza kubadilika toka ubeti
wa kwanza hadi ubeti wa pili wa shairi na
kubadilika huku
kunaitwa kimalizio. TUKI (2003:94), wameandika kuwa: kituo ni mstari wa mwisho
katika kila ubeti wa ushairi. Kituo huweza kuwa kimalizio au kiini. Kina kuwa
kimalizio kinapokuwa kuwa kinatumiwa kama kitu
cha kulifunga na kulikamilisha wazo moja katika kila ubeti. Kina kuwa kiini
inapokuwa kikitumiwa na kikijitokeza
katika kila mwisho wa ubeti na kinataja kwa muhtasari jambo muhimu
linalozungumziwa.
Mfano: (Kapele
H. 2013),
Mke bwana mtafute, popote upajuapo,
Tia nia umpate, usikwepe ya malipo,
Raha ya ndoa fungate, fungate pasi
mkopo,
Mke
usije kupewa, matusi atakutia.
Mke ni yako zawadi, zawadi ya
boksini,
Hata kiwa mkaidi, ya ndoa yote
sirini,
Hata akiwa ni udi, usitangaze
mbaoni,
Mke
usije kupewa, matusi atakutia.
Kituo kimetiwa
wino mzito.
- kibwagizo
ni mstari wa mwisho wa ubeti unaorudiwa
katika kila ubeti wa shairi lote, pia
kwa lugha nyingine waweza kuitwa mkarara,
kipokeo au kiitikio. Huweza kuwa
kipande kinachorudiwa katika mshororo wa
mwisho wa ubeti. Kazi ya
kibwagizo katika ushairi yaweza kuwa ni
kusisitiza jambo ambalo msanii na
mtunzi wa shairi amelenga jamii iweze
kulisoma, kulisikia, kulifanya na kuamua pia
kibwagizo hueleza
dhamira muhimu ya shairi katika mengi ndicho huwa kiini na kichwa cha shairi.
Mfano: TUKI
(2003:103)
Buibui ndugu yangu, si numba
uliyo nayo,
Kwani naona uchungu, kwa maisha
uishivyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.
Nyumba iso mlingoti, na wala
vipachikiyo,
Toka pembe hadi kati, yote ya
mning’iniyo,
Haiezekwi makuti, na wala
kifunikiyo,
Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina
stara.
Katika beti
hizi kibwagizo kimekolezwa kwa wino zaidi.
- kimalizio
ni mstari wa
mwisho katika ubeti ambao haurudiwi katika kila ubeti, mstari huu hufanya kazi
ya kukuamilisha wazo lililo katika ubeti wa shairi.
- kipande
ni mgao au kisehemu
kimojawapo katika visehemu viwili au vitatu vya mshororo
ambavyo
hutenganishwa kwa kituo au alama ya mkato mwishoni mwa kipande cha kina. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa:
kipande ni kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au zaidi vya kila mstari
kwa tungo zenye kugawanyika katika sehemu mbili au zaidi katika kila mstari.
Mfano:
kila usilolijuwa,
kujifunza ni wajibu,
Ndipo utapo tambuwa,
japokuwa taratibu,
Papara kuiondowa, ili
usije haribu,
Bila shaka utaswibu, ile haja
utakayo.
Katika ubeti huu
kuna vipande viwili ambavyo ni ukwapi na utao.
- ukwapi
ni
kipande cha kwanza cha mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
Ukwapi umekolezwa vizuri ili uweze kuonekana
vuzuri.
- Utao
ni kipande cha pili katika mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu. Utao umekolezwa vizuri.
- mwandamizi
kipande cha tatu
katika mshororo.
Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
Mwandamizi umokolezwa ili kuonekana vizuri.
- mizani
ni silabi
zilizomo katika kila mshororo wa shairi huleta urari wa mapigo katika shairi, arudhi huwa na idadi ya mizani
inayolingana. Wamitila (2010:218), anaeleza kuwa mizani ni silabi zinazo tamkika. TUKI (2003:94), mizani
ni jumla ya silabi zilizomo katika kila mstari wa ubeti. Wanafafanua kuwa
katika ushairi hizi ndizo ziletazo urari wa mapigo, kwani kila mstari watakiwa
uwe na mizani sawa na mistari mingine au wakati mwingine ule mstari wa mwisho
uwe na nusu ya mizani ya mstari mmoja. Mashairi yana vipimo vinavyopima urefu
wa kira mstari. Vipimo hivyo huitwa mizani, kila silabi moja Tazama mfano kutoka katika shairi hili; mtunzi
(kapele. H, 2013)
mja deni utalipa,
hata likiwa ni mia,
dawa ya deni kulipa,
wala siko kukimbia,
deni harusi kukopa,
kulipa wafikiria,
ili moyo uwe shwari,
mja kamilisha deni.
Katika shairi
hili mizani iko kumi na sita ambayo inaweza kuonekana hivi na kuhesabika kwa
urahisi.
M ja
de ni u ta li pa,
ha ta
li ki wa
ni mi a,
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16
- urari wa mizani
ni mpangilio wa
idadi ya mizani katika mstari au mshororo mmoja wa shairi. Katika mashairi ya
tarbia (unne), kwa kawaida kuna mizani kumi na sita. Katika tungo za aina
nyingine vipande na mistari huwa na idadi tofauti ya mizani. Mizani yaweza kuwa
irabu moja, konsonanti moja, konsonanti moja na irabu, konsonanti mbili na irabu,
konsonanti tatu na irabu. TUKI (2003:104) wanaeleza kuwa:
urari ni
mpangilio wa mistari ya ubeti. Yaani unaweza kuusoma ubeti halafu ukasema
mstari huu wa pili ungekuwa wa kwanza na huu wa kwanza ungekuwa wa pili.
- kina
ni sauti ya silabi
iliyomwishoni mwa mshororo au kipande cha sauti, kuangalia vina tunakuta kuna
aina mbili ambazo kina cha ndani na kina nje au kina
kati na kina
mwisho. Baadhi ya mashairi yana vina vya kati na vin avya mwisho, yaani
mshororo huwa umegawanyika sehemu mbili, kila sehemu ikiitwa kipande.
Mfano: hebu
tuangalie vina katika shairi lifuatalo, wamitila (2010:218), yeye anaeleza kuwa
vina ni silabi zinazofanana na ambazo hupatikana katika sehemu moja katika
mpangilio wa shairi. TUKI (2003:93), wanaeleza kuwa vina ni zile mizani za kati
na za mwisho au pengine za mwisho tu
zenye kufanana katika kila mstari wa ubeti, na katika tarbia aghalabu
vina hufanana katika ile mistari mitatu ya mwanzo tu, mwanzo, mroto, na mleo. Tazama mfano huu (Kapele. H, 2013)
Tulipofika mpanda, tulizani njia panda,
Tuliendelea panda,
tukaufika uwanda,
Alikozaliwa pinda,
mnyoosha walopinda,
Hongera waziri panda,
sasa twaweza pumua.
TUKI (2003)
Mkono inuka, inuka hima, twaa
kalamu,
Upate yandika, kwa khati njema,
hino nudhumu,
Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
Wapate yashika, nakuyapima,
yalipo humu.
Katika ubeti huu
ambao ni mfano mzuri wa shairi la kimapokeo lenye sifa ya tarbia yaani unne
vina vimekolezwa wino na kuonekana wazi. Vina kati ni nda na vina mwisho ni nda.
Laini katika mshororo wa mwisho kina kati ni nda na kina mwisho ni a
- utoshelezi
katika kujadili
utoshelezi waandishi wengi wanaeleza kuwa lazima kila ubeti huitaji kuwa na
maana inayojitosheleza au kujisimamia
bila kutegemea ubeti unaotangulia au unaofuata hapohapo na kuwa na mtiririko
mzuri wa habari inayoelezwa. TUKI (2003:105) wanasema utoshelezo katika shairi
la Kiswahili ni lile ambalo kila ubeti unajitosheleza kamili kwa habari au
ujumbe unaompa msomaji ili afahamu wamweleza nini katika ubeti ule, halafu
uendelee na ubeti mwingine ukiwa katika mtiririko wa habari yako unayoieleza
huku ukiwa mwenye kufuata mpango uleule wa kila ubeti kujitosheleza mpaka
mwisho wa shairi lako.
- muwala
ni mtiririko wa
fani n amawazo ulion amantiki katika shairi, katika taaluma hii ya ushairi kuna
aina mbili za muwala yaani mawazo y aubeti yawe yanafuatana kwa ufasaha kutoka
fatahi, mroto, mleo na kituo ili kuyajenga mawazo kikamilifu. Aina ya pili au
sheria muwala lazima uwe na mtiririko mzuri wa mawazo kutoka ubeti hadi ubeti
katika aina hii mawazo huwa yamefungamana na maudhui ya tungo huwa
yamekamilika. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa muwala ni ile hali ya utoshelevu
katika ubeti hadi ubeti katika utungo mzima, yaani kilaheleza katika maana
lakini wakati huo huo ukawa hausigani na beti nyingine. Mfano ubeti wa
utangulizi wa shairi hauwezi ukawa kati ya utungo. Tazama (Kapele. H, 2013)
hodi hodi naingia, uwanjani
kwa kishindo,
uwanja naufagia, machafu
kuweka kando,
watu wote shangilia,
taratibu wangu mwendo,
kinda manua mdomo, chakula
utapikiwe.
Ubeti
huu ni mwanzo wa utungo unafaa kuwekwa mwanzo ili kujua utangulizi wa utungo.
"MTI UKULIAO KIVULINI SI THABITI"
12 comments:
Nice
nzuri sana
Dole 😂
Big up
Safi👏🏼
Safi sana mwanagenzi
Safi
Iko vzr
Nice lesson
Sijaelewa kwenye kituo...
Hivi kituo ni lazima uwe mstari wa mwisho?? Na vipi kuhusu kingekuwa mwanzo hatuiti kituo???
Ingependeza tufasiri kituo ni mstari unaojirudia rudia ktk kila ubeti na waweza kuwa mwanzo kati au mwisho
Naomba kufahamishwa vipegele vya muwala
Be blessed thanks
Post a Comment