Saturday, June 22, 2013

ISTILAHI ZA USHAIRI


ISTILAHI ZA USHAIRI  -  tarehe 9/5/2013


MAANA YA ISTILAHI
Ni maneno yanayotumiwa katika tathinia fulani, hivyo katika taaluma ya ushairi kuna istilahi muhimu zitumikazo katika kuunda na kujenga ushairi wa Kiswahili. Istilahi hizo ni:

  1. Arudhi
      Ni sheria na kanuni za kimapokeo, jadi au kitamaduni zinazoongoza utunzi
      wa mashairi, tenzi, na ngonjera. Kanuni hizo zaweza kuwa ni vina, mizani,
      beti, mishororoau mistari, kituo, kibwagizo, mikarara, utoshelevu, muwala
      na lugha safi.

  1. Bahari
      Ni kina kinachotokeza mwishoni mwa mshororo wa beti.

  1. Ubeti
      Ni mgawo wa vifungu katika shairi, utenzi, au ngonjera unaojitosheleza
kimaana. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa: ubeti ni kifungu chenye kuleta     maana kamili katika jumla ya vifungu vilivyomo katika utungo.
Mfano:
           Kaa kaa kwenye kiti, kaa na kaa wa pwani,
           Kaa ni la moto binti, nisikiza kwa makini,
           Kaa waambiwa keti, ewe bwana una nini?
Huu ni ubeti mmoja katika utungo wa shairi letu kutoka katika Mzenga, (2010:4)

  1. mshororo
      ni mstari katika ubeti wa shairi ambao una maana kamili. Katika mashairi
      ya arudhi inatakiwa mistari iwe sawa kimizani ingawa baadhi ya mashairi
      huwa yanakuwa na mizani tofauti.
      Mfano:
                  Paa ni la kuezeka, kwenye nyumba pulikani.
      Huu ni mshororo mmoja wenye mizani kumi na sita.

  1. mwanzo
      ni mshororo wa kwanza katika ubeti wa shairi. Katika tarbia mshororo wa
kwanza huitwa ufunguo au fatahi au kifunguo.
             
               Buibui ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
               Kwani naona uchungu, kwa maisha uishivyo,
               Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.

                Nyumba iso mlingoti, na wala vipachikiyo,
                Toka pembe hadi kati, yote ya mning’iniyo,
                Haiezekwi makuti, na wala kifunikiyo,
                Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.
Ubeti wenye wino mzito ni mfano wa mwanzo wetu katika utungo wetu.

  1. mloto
      ni mshororo wa pili katika ubeti wa ushairi.
       Mfano:
               Buibui ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
               Kwani naona uchungu, kwa maisha uishivyo,
Mstari wenye wino mzito kishairi huo ni mroto.


  1. mleo
      ni mshororo wa tatu katika ubeti wa shairi.
      Mfano:
        mja deni utalipa, hata likiwa ni mia,
        dawa ya deni kulipa, wala siko kukimbia,
        deni harusi kukopa, kulipa wafikiria,
        ili moyo uwe shwari, mja kamilisha deni.
   Mleo umekolezwa zaidi ya mishororo mingine katika ubeti.


  1. kituo
            ni mshororo wa mwisho katika ubeti wa utungo wa ushairi. Maneno ya kituo
            yanaweza yakawa yale yanayokaririwa katoka ubeti hadi ubeti yaani kibwagizo.
            Pia yanaweza kubadilika toka ubeti wa kwanza hadi ubeti wa pili wa shairi na
kubadilika huku kunaitwa kimalizio. TUKI (2003:94), wameandika kuwa: kituo ni mstari wa mwisho katika kila ubeti wa ushairi. Kituo huweza kuwa kimalizio au kiini. Kina kuwa kimalizio kinapokuwa kuwa kinatumiwa kama kitu cha kulifunga na kulikamilisha wazo moja katika kila ubeti. Kina kuwa kiini inapokuwa kikitumiwa  na kikijitokeza katika kila mwisho wa ubeti na kinataja kwa muhtasari jambo muhimu linalozungumziwa.
Mfano: (Kapele H. 2013),
         
          Mke bwana mtafute, popote upajuapo,
          Tia nia umpate, usikwepe ya malipo,
           Raha ya ndoa fungate, fungate pasi mkopo,
           Mke usije kupewa, matusi atakutia.
    
           Mke ni yako zawadi, zawadi ya boksini,
           Hata kiwa mkaidi, ya ndoa yote sirini,
           Hata akiwa ni udi, usitangaze mbaoni,
           Mke usije kupewa, matusi atakutia.
Kituo kimetiwa wino mzito.    

  1. kibwagizo
      ni mstari wa mwisho wa ubeti unaorudiwa katika kila ubeti wa shairi lote, pia
      kwa lugha nyingine waweza kuitwa mkarara, kipokeo au kiitikio. Huweza kuwa
      kipande kinachorudiwa katika mshororo wa mwisho wa ubeti. Kazi ya
      kibwagizo katika ushairi yaweza kuwa ni kusisitiza jambo ambalo msanii na
      mtunzi wa shairi amelenga jamii iweze kulisoma, kulisikia, kulifanya na kuamua pia
kibwagizo hueleza dhamira muhimu ya shairi katika mengi ndicho huwa kiini na  kichwa cha shairi.
Mfano: TUKI (2003:103)
               Buibui ndugu yangu, si numba uliyo nayo,
               Kwani naona uchungu, kwa maisha uishivyo,
               Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.

                Nyumba iso mlingoti, na wala vipachikiyo,
                Toka pembe hadi kati, yote ya mning’iniyo,
                Haiezekwi makuti, na wala kifunikiyo,
                Hiyo nyumba ukaayo, kamwe haina stara.
Katika beti hizi kibwagizo kimekolezwa kwa wino zaidi.

  1. kimalizio
ni mstari wa mwisho katika ubeti ambao haurudiwi katika kila ubeti, mstari huu hufanya kazi ya kukuamilisha wazo lililo katika ubeti wa shairi.

  1. kipande
            ni mgao au kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au vitatu vya mshororo
ambavyo hutenganishwa kwa kituo au alama ya mkato mwishoni mwa kipande  cha kina. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa: kipande ni kisehemu kimojawapo katika visehemu viwili au zaidi vya kila mstari kwa tungo zenye kugawanyika katika sehemu mbili au zaidi katika kila mstari.
Mfano:
             kila usilolijuwa, kujifunza ni wajibu,
             Ndipo utapo tambuwa, japokuwa taratibu,
             Papara kuiondowa, ili usije haribu,
             Bila shaka utaswibu, ile haja utakayo.
Katika ubeti huu kuna vipande viwili ambavyo ni ukwapi na utao.

  1. ukwapi
      ni kipande cha kwanza cha mshororo.
             Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
             Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
             Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
             Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
Ukwapi umekolezwa vizuri ili uweze kuonekana vuzuri.


  1. Utao
      ni kipande cha pili katika mshororo.            
              Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
              Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
              Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
              Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu. Utao umekolezwa vizuri.
                   
  1. mwandamizi
kipande cha tatu katika mshororo.
              Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
              Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
              Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
              Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.
          Mwandamizi umokolezwa ili kuonekana vizuri.

  1. mizani
ni silabi zilizomo katika kila mshororo wa shairi huleta urari wa mapigo katika     shairi, arudhi huwa na idadi ya mizani inayolingana. Wamitila (2010:218), anaeleza kuwa mizani ni  silabi zinazo tamkika. TUKI (2003:94), mizani ni jumla ya silabi zilizomo katika kila mstari wa ubeti. Wanafafanua kuwa katika ushairi hizi ndizo ziletazo urari wa mapigo, kwani kila mstari watakiwa uwe na mizani sawa na mistari mingine au wakati mwingine ule mstari wa mwisho uwe na nusu ya mizani ya mstari mmoja. Mashairi yana vipimo vinavyopima urefu wa kira mstari. Vipimo hivyo huitwa mizani, kila silabi moja  Tazama mfano kutoka katika shairi hili; mtunzi (kapele. H, 2013)
                           mja deni utalipa, hata likiwa ni mia,
                           dawa ya deni kulipa, wala siko kukimbia,
                           deni harusi kukopa, kulipa wafikiria,
                           ili moyo uwe shwari, mja kamilisha deni.
Katika shairi hili mizani iko kumi na sita ambayo inaweza kuonekana hivi na kuhesabika kwa urahisi.
                           M   ja  de  ni  u  ta   li   pa,   ha  ta    li    ki   wa   ni   mi     a,
                                        1   2   3   4    5   6   7   8     9   10   11   12   13    14   15    16

  1. urari wa mizani
ni mpangilio wa idadi ya mizani katika mstari au mshororo mmoja wa shairi. Katika mashairi ya tarbia (unne), kwa kawaida kuna mizani kumi na sita. Katika tungo za aina nyingine vipande na mistari huwa na idadi tofauti ya mizani. Mizani yaweza kuwa irabu moja, konsonanti moja, konsonanti moja na irabu, konsonanti mbili na irabu, konsonanti tatu na irabu. TUKI (2003:104) wanaeleza kuwa:
urari ni mpangilio wa mistari ya ubeti. Yaani unaweza kuusoma ubeti halafu ukasema mstari huu wa pili ungekuwa wa kwanza na huu wa kwanza ungekuwa wa pili.

  1. kina
ni sauti ya silabi iliyomwishoni mwa mshororo au kipande cha sauti, kuangalia vina tunakuta kuna aina mbili ambazo kina cha ndani na kina nje au kina
kati na kina mwisho. Baadhi ya mashairi yana vina vya kati na vin avya mwisho, yaani mshororo huwa umegawanyika sehemu mbili, kila sehemu ikiitwa kipande.
Mfano: hebu tuangalie vina katika shairi lifuatalo, wamitila (2010:218), yeye anaeleza kuwa vina ni silabi zinazofanana na ambazo hupatikana katika sehemu moja katika mpangilio wa shairi. TUKI (2003:93), wanaeleza kuwa vina ni zile mizani za kati na za mwisho au pengine za mwisho tu  zenye kufanana katika kila mstari wa ubeti, na katika tarbia aghalabu vina hufanana katika ile mistari mitatu ya mwanzo tu, mwanzo, mroto,  na mleo. Tazama mfano huu (Kapele. H, 2013)

             Tulipofika mpanda, tulizani njia panda,
              Tuliendelea panda, tukaufika uwanda,
              Alikozaliwa pinda, mnyoosha walopinda,
              Hongera waziri panda, sasa twaweza pumua. 
           
             TUKI (2003)
              Mkono inuka, inuka hima, twaa kalamu,
              Upate yandika, kwa khati njema, hino nudhumu,
              Ipate someka, mwenye kusoma, wahifahamu,
              Wapate yashika, nakuyapima, yalipo humu.


            
Katika ubeti huu ambao ni mfano mzuri wa shairi la kimapokeo lenye sifa ya tarbia yaani unne vina vimekolezwa wino na kuonekana wazi. Vina kati ni nda na vina mwisho ni nda. Laini katika mshororo wa mwisho kina kati ni nda na kina mwisho ni a

  1. utoshelezi
katika kujadili utoshelezi waandishi wengi wanaeleza kuwa lazima kila ubeti huitaji kuwa na maana  inayojitosheleza au kujisimamia bila kutegemea ubeti unaotangulia au unaofuata hapohapo na kuwa na mtiririko mzuri wa habari inayoelezwa. TUKI (2003:105) wanasema utoshelezo katika shairi la Kiswahili ni lile ambalo kila ubeti unajitosheleza kamili kwa habari au ujumbe unaompa msomaji ili afahamu wamweleza nini katika ubeti ule, halafu uendelee na ubeti mwingine ukiwa katika mtiririko wa habari yako unayoieleza huku ukiwa mwenye kufuata mpango uleule wa kila ubeti kujitosheleza mpaka mwisho wa shairi lako.

  1. muwala
ni mtiririko wa fani n amawazo ulion amantiki katika shairi, katika taaluma hii ya ushairi kuna aina mbili za muwala yaani mawazo y aubeti yawe yanafuatana kwa ufasaha kutoka fatahi, mroto, mleo na kituo ili kuyajenga mawazo kikamilifu. Aina ya pili au sheria muwala lazima uwe na mtiririko mzuri wa mawazo kutoka ubeti hadi ubeti katika aina hii mawazo huwa yamefungamana na maudhui ya tungo huwa yamekamilika. TUKI (2003:94), wanaeleza kuwa muwala ni ile hali ya utoshelevu katika ubeti hadi ubeti katika utungo mzima, yaani kilaheleza katika maana lakini wakati huo huo ukawa hausigani na beti nyingine. Mfano ubeti wa utangulizi wa shairi hauwezi ukawa kati ya utungo. Tazama (Kapele. H, 2013)
                   hodi hodi naingia, uwanjani kwa kishindo,
                   uwanja naufagia, machafu kuweka kando,
                   watu wote shangilia, taratibu wangu mwendo,
                   kinda manua mdomo, chakula utapikiwe.

Ubeti huu ni mwanzo wa utungo unafaa kuwekwa mwanzo ili kujua utangulizi  wa utungo.

                                  "MTI UKULIAO KIVULINI SI THABITI"


12 comments:

Unknown said...

Nice

Unknown said...

nzuri sana

Unknown said...

Dole 😂

DOTTO MOSSES NYAMKINDA said...

Big up

Unknown said...

Safi👏🏼

Unknown said...

Safi sana mwanagenzi

Unknown said...

Safi

Unknown said...

Iko vzr

Unknown said...

Nice lesson

Unknown said...

Sijaelewa kwenye kituo...
Hivi kituo ni lazima uwe mstari wa mwisho?? Na vipi kuhusu kingekuwa mwanzo hatuiti kituo???
Ingependeza tufasiri kituo ni mstari unaojirudia rudia ktk kila ubeti na waweza kuwa mwanzo kati au mwisho

Unknown said...

Naomba kufahamishwa vipegele vya muwala

Unknown said...

Be blessed thanks